Agnes Masogange ahukumiwa kwenda Jela miaka 2

Video vixen Agnes Gerald akijulikana sana kama Agnes Masogange amepatikana na hatia hatia na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kuhukumiwa miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 baada ya kukutwa na madawa ya kulevya  aina ya Oxazepam.

Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri ametoa hukumu hiyi Leo na kuieleza mahakama kuwa amekutwa na hatia katika makosa yote mawili.
Hivyo katika kosa la kwanza mahakama inamuhukumu kwenda jela kwa miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni moja na kosa la pili amehukumiwa kwenda jela miezi kumi na mbili au kulipa faini ya shilingi laki tano”.
February 17 mwaka Jana Agnes Masogange alitiwa hatiani kwa tuhuma za kutumia madawa ya kulevya ambapo alienda kupimwa na mkemia mkuu Wa serikali.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment