Idara ya Uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi Abdul Nondo Asema Mh.Zitto Kabwe

Ni mbunge wa Kigoma mjini Mh.Zitto kabwa ambaya kupitia kurasa yake ya mitandao ya kijamii ameelezea jinsi Idara ya uhamiaji inavyotumika kisiasi dhini ya mwanafunzi na raisi wa TSNP Abdul Nondo,na kwamba sio kosa kwa mwanafunzi huyo kuzaliwa Kigoma Ujiji .


Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini ( Jimbo analotoka Abdul na wazazi wake na mababu zake).
Idara ya Uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania. Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji na Serikali ya Awamu ya awamu ya Tano kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment