Maua Sama Asema Kilichomtokea Nandy kinaweza Kumtokea Yoyote

Bongo nzima imechafuka na sasa stori ni moja tu nchi nzima ,Baada ya Video na picha kusambaa ikimuhusisha Nandy na Bill Nass wakiwa faragha .

Msanii Maua Sama akiwa katika  mahojiano na Kipindi cha 5 Selekt, EATV amesema kwamba tukio kama hilo linaweza  kumtokea mtu yeyote na anaamini video hiyo imesambaa kwa bahati mbaya.
“Nafikiri ile ni bahati mbaya inaweza kumtokea mtu mwingine yeyote japokuwa i cant say much lakini mimi naona kama imetokea bahati mbaya,” amesema Maua Sama.
 Jana Nandy aliomba radhi kwa mashabiki wake kwa kile kilichotokea kupitia ukurasa wake wa instagram aka andika 
Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi SANA SANA familia yangu, Ndugu zangu, Mashabiki wangu na Serikali kwa kilochotokea, bado siko sawa.. naomba mniombee uzima.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment