Mbowe na wenzake wapata dhamana

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri amewapa dhamana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano .


Mashauri amesema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi kwa masharti ya kusaini bondi ya Sh. 20 milioni kila mmoja pamoja na wadhamini wawili.

Viongozi hao wa 5 waliokua mahabusu ni pamoja na Freeman Mbowe,Vincent Mashinji Naibu katibu Mkuu Bara,John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Wamepata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20.
abla ya kutoa uamuzi huo Hakimu Mashauri alipinga madai ya magereza ya kushindwa kuwaleta washtakiwa mahakamani kwa madai ya kuharibikiwa na gari, hivyo alilazimika kutoa uamuzi bila ya yao kuwepo na taratibu nyingine zitafuata.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment