Mchuano wa Daimond na Alikiba huko Rwanda

 Jean Baptiste Nyabyenda ni Muandaaji wa Filamu na Mwandishi wa Habari kutoka Rwanda,alielezea   hali halisi ilivyo ya muziki wa Bongo Fleva nchini Rwanda, ambapo amekiri wazi kuwa muziki huo unapendwa na unapigwa sana kwenye Media nchini Rwanda.


Akizungumza na Bongo5, Jean amesema kuwa licha ya muziki huo kupigwa zaidi kwenye Media lakini wasanii wanaopigwa zaidi ni Alikiba na nyimbo za wasanii kutoka WCB.

Jean amesema nyimbo za Alikiba zinapigwa kwa kiasi kikubwa lakini ngoma za wasanii wa WCB ndio zinazotawala zaidi kwenye Radio/TV na hata kwenye kumbi za starehe.

Kwa upande mwingine, Jean amedai kuwa wapo wasanii wengine kama A.Y, Mr. Nice, Mr. Blue nao nyimbo zao zinapigwa lakini sio kama za wasanii hao aliyowataja. 

Habari ::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment