"Mimi ni Mtu Mzima Najua Nachofanya"MremboTunda

Mlimbwende Tunda ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na urembo wake, amefunguka na kuwataka watu waache tabia ya kumfuatilia juu ya maisha yake binafsi anayoishi bali waangalie na kufuatilia kile anachokuwa amekiweka katika mitandao nasio vinginevyo.


Tunda ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya watu wengi kujiuliza maswali mengi vichwani mwao huku wengine wakienda moja kwa moja kumuuliza yeye mwenyewe kuhusiana na kazi gani ambayo anaifanya kubwa ambayo kila uchao inamfanya ale bata sehemu zenye hadhi kubwa kila uchao.

"Mimi napenda kuwaambia hao watu, wafuatilie vile ambavyo nimeamua kuviweka wazi na vile ambavyo sijaamua kuviweka bayana basi waachane navyo. Msitake kumuingia mtu kiundani sana 'some times' inakuwa ina boa, endapo nitaona sasa biashara yangu inafaa kuiweka kwenye mitandao nitaweka na kama sijaiweka waache na wanyamaze wanifuatilie mimi ninachokifanya", amesema Tunda.

Pamoja na hayo, Tunda ameendelea kwa kusema "mimi ni mtu mzima najua ninachokifanya. Sio kila ninachokifanya instagram ndio maisha yangu yote, nina maisha yangu mengine ambayo hayapo katika mitandao ya kijamii".

ra
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment