Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la #RaiaMwema Kuhojiwa kwa kuandika makala yenye kichwa kisemacho "Bunge linajipendekeza?"Spika Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Maadili ya Bunge, kumhoji Mwanahabari Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la #RaiaMwema kwa kuandika makala yenye kichwa kisemacho "Bunge linajipendekeza?"
-
Makala hiyo iliyochapishwa katika gazeti toleo Na. 556 la Aprili 9-10, 2018 inadaiwa kulidhalilisha Bunge
-
Moja ya masuala aliyoongelea mwandishi katika makala hiyo ni yeye kuliona Bunge la Tanzania kuwa ‘Butu’, ambapo aliandika "Naomba kuuliza swali dogo kuhusu Bunge letu, kuna wakati enzi za Spika Samwel Sitta Bunge la Tanzania lilipata meno, lakini sasa, ni mimi tu naliona kama kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuwa Bunge butu, Bunge kibogoyo. Je, litaweza kweli kuisimamia Serikali?"
Habari ::Jamiiforum 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment