Sakata la wanawake waliotelekezwa Linaloendeshwa na RC Makonda Lakosolewa na Naibu Waziri wa Afya amkosoa

Hili sakata la Wanawake waliotelekezwa na wazazi wenzao linawadhalilisha watoto na linahitaji kukemewa kama Dkt,Faustine Ndugulile Naibu Waziri wa Afya alilivyolikemea kwa nguvu,Sababu watoto hawa wana sheria zinazowalinda na sura zao zinatakiwa kufichwa wakati kwenye zoezi hili imekua sivyo picha zo zimekua zikishambaa katika mitandao ya kijamii tena wengine na kejeli wanatoa.

Zoezi hili la watoto na mama zao waliotelekezwa linaendelea pale kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda .
Kukemea kwa Dkt Faustine kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ametumia nafasi yake kuvionya vyombo vya habari kwa kushiriki kuonyesha picha za watoto katika mikusanyiko hiyo, huku akitaka utaratibu ufuatwe katika kusikiliza mashauri ya walalamikaji ikiwa ni pamoja na usiri;
Ni kosa kisheria kwa chombo cha habari au mitandao ya jamii kuonyesha picha zenye kumdhalilisha mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto Namba 21 ya 2009. Navikumbusha vyombo vya habari kulinda haki za watoto na kutokuwa washirika katika kudhalilisha haki za watoto.
Ushauri wangu kama Wizara inayosimamia haki za watoto, suala kama hili linapaswa kufanyika kwa faragha, kwa sababu una deal na watu na litakuwa endelevu
Anachokifanya Makonda ni jambo zuri, lakini linahitaji uangalifu na tufuate mifumo sahihi. Nitoe rai kwa wananchi wote kufuata taasisi zinazohusika.
Alipoulizwa sababu ya wananchi wengi kujitokeza kwa mkuu wa mkoa kama ishara ya kuzidiwa kwa idara ya Ustawi wa Jamii, Dk Ndugulile alikanusha na kueleza;
Si kwamba Ustawi wa Jamii umezidiwa, inawezekana wananchi hawana taarifa za kutosha kwa hiyo kupitia mikutano kama hiyo watapata taarifa. Tufuate mifumo rasmi inayokubalika kisheria.
Hapo jana Mamia ya wanawake waliotelekezwa ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na wazazi wenzio, pia RC Makonda alitoa nafasi ya kuwasikiliza wanaume waliotelekezwa na wake zao huku akiahidi kuwapa msaada wa kisheria ili wasaidiwe kama wanavyosaidiwa wanawake.
Habari :Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment