Serikali Imekubali kwamba kuna Changamoto ya Wajawazito Kulala Kitanda Kimoja

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imekiri kuwepo kwa changamoto ya wakina mama wajawazito kulala katika kitanda kimoja hospitali.
Akizungumza jana Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Kenani aliyehoji
Katika hospitali ya rufaa ya Rukwa kumekuwepo na tatizo la wanawake wajawazito na wanaojifungua kulala katika kitanda kimoja, Je serikali ina mkakati gani katika kumaliza tatizo hilo?
“Ni kweli kumekuwa na Changamoto ya wakina mama Wajawazito kulala katika kitanda kimoja hali inayochangia ufinyu wa nafasi katika jengo la wazazi lililopo kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wa huduma hizi hasa kwa kuwa hospitali hii iklianza kama kituo cha afya mwaka 1974 vilevile tatizo hili linatokana na ukosefu wa hospitali za Wilaya katika Halmashauri za Kalambo na Sumbawanga hali inayosababishwa hali inayopelekea hospitali ya mkoa kuhudumia wateja wote wanaotoka hospitali zote mbili,” amesema Dkt. Faustine.
“Wizara imeweka ufunguzi wa changamoto hii kama ifuatavyo kupitia mpango kabambe wa hospitali kwa mwaka 2017/2018 wizara imekamilisha wodi mbili na hivyo kuongeza na hivyo kuongeza vitanda vya ziada 20 ambavyo tayari vinatumika na hivyo kupunguza msongamano uliokuwepo.”
Story Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment