Ali Kiba Amchagua Mpoki kama Msemaji wa Kikosi chake cha Mpira

Katika kuelekea mchezo maalumu wa hisani ya kuchangia elimu, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ametangaza kikosi cha wachezaji watakao kuwa upande wake kupambana dhidi ya  kikosi cha wachezaji watakaokuwa upande wa mshambuliaji wa timu ya Taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta.


Kwenye kikosi hicho, Alikiba amemchukua mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi na wachezaji wengine kama John Bocco, Msuva, Erasto Nyoni, Abdu Kiba na wengineo kama inavyoonesha hapa chini kwenye picha.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mnamo Juni 9, 2018 .
Source::bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment