Ali Kiba nae Kupelekwa Mahakamani Kisa Matunzo ya Mtoto

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ali kiba nae amaeingia kwenye issue ya kushtakiwa kisa hatoi matunzo ya mtoto ,na  ameshtakiwa mahakamani na mzazi mwenzie aliyejitambulisha kwa jina la Hadija kwa kosa la kushindwa kutoa matunzo kwa mtoto wake wa miaka mitano.

Bi. Hadija ambaye ni mfanyabiashara wa mitumba amesema amefungua kesi ya madai ya matunzo katika Mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo amesema anamdai Alikiba kiasi cha milioni 1.4 kwa ajili ya matumizi ya mtoto.
Akifafanua gharama hizo, Hadija amesema kuwa anamdai Alikiba tsh 950,000/= za ada na kiasi cha tsh 460,000/= kwa ajili ya matumizi ya mtoto huyo wa kike ambaye ana umri wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, mlalamikaji Bi. Hadija anadai kuwa Januari 2013 katika Hospitali ya Mikocheni jijini Dar es salaam alizaa mtoto wa kike (jina lake limehifadhiwa) na baba yake ni mlalamikiwa (Alikiba).
Kupitia hati hiyo, mlalamikaji anadai kuwa Alikiba anapaswa kulipia gharama zote za mahitaji muhimu kwa mtoto huyo ikiwemo chakula, nguo, elimu na matibabu.
Kutokana na sheria ya watoto ya mwaka 2009, mdaiwa anatakiwa kutoa huduma kila mwezi. Chakula laki 150,000/=, matunda 50,000/=, chakula cha ziada 50,000/=, michezo na burudani kwa watoto 100,000/=, nguo tsh 60,000/= na matibabu tsh 50,000/= ambapo jumla ni Tsh 460,000/=.“ameeleza Bi. Hadja .
Bi. Hadja pia ameiomba mahakama kuwa Mlalamikiwa alipe kiasi cha tsh 460,000/= kila mwezi tangu alipoacha kutoa huduma mwezi februari 2017 na kiasi cha tsh 950,000/= kwa ajili ya ada ya mtoto kwa muhula mmoja.
Mbali na maombi hayo, Bi. Hadija anaiomba mahakama itoe amri nyingine yoyote ile itakayoona inafaa kwa manufaa yake. kesi hiyo imefunguliwa kwa msaada wa kituo cha wanawake cha msaada wa kisheria (WLAC).
Wiki mbili zilizopita Alikiba alifunga ndoa na mchumba wake Aminah kutoka Mombasa nchini Kenya, ambapo sherehe za pili za harusi hiyo zilikuja kufanyika jijini Dar es salaam Aprili 29, 2018 katika Hoteli ya Serena.
Chanzo:Nipashe,Bongo 5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment