'' Flaviana Matata ni mfano wa kuigwa na Vijana'' Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza Mwanamitindo wa Kimataifa, Flaviana Matata kwa juhudi za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha vifaa muhimu vya shule ikiwemo ada na madaftari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.
“Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata” ameongeza Dkt. Mwakyembe.
Aidha, aliongeza kwa kueleza kuwa, Mwanamitindo huyo amekuwa ni Balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amempongeza Bibi. Flaviana kwa kuwa mfano bora kwa watoto wa kike kwa jinsi ambavyo amekuwa akisaidia watoto wa kike nchini.
Naye Mwanamitindo,Flaviana ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.
Hata hivyo, Mwanamitindo huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa jitihada za wazi wanazozifanya katika kusimamia haki za wasanii na hivyo kurudisha hadhi ya tasnia hiyo nchini.
Source::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment