Mh.Joseph Mbiliny aka Sugu Asema Jeshi la Magereza lina hali mbaya sana

Mbunge wa Mbunge Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema kuwa Jeshi la magereza lina hali mbaya, halina magari na magari yaliyopo ni mabovu.

Leo, Mei 22 Bungeni jijini Dodoma, Sugu ameyasema hayo wakati akiuliza swali wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, lililojibiwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, ambapo amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo inapelekea watuhumiwa kufungwa pingu kutembea kwa miguu mtaani hali inayopelekea kuhatarisha maisha ya mfungwa.

Sugu aliuliza “Pamoja na matatizo waliokuwa nayo Polisi, kwenye masuala ya vyombo vya usafiri lakini nikuhakikishie Jeshi la Magereza lina hali mbaya sana hawana magari sio tu magari mabovu kiasi kwamba wanafikia kupeleka kupeleka wafungwa ambao wana kesi au rufaa wanawafunga pingu wanawapeleka mahakamani kwa miguu sasa hii ni mbaya sana kwa usalama wao na wale Askari magereza lakini pia kwa wao kwa wale watuhumiwa ambao wamefungwa pingu na kutembezwa kwa miguu kwasababu madhalani anatuhumiwa ujambazi alafu anapita mtaani wale wanaomtuhumu wanamuona wanaweza wakamshambulia na kuhatarisha maisha ya yule mfungwa?, alihoji Sugu.

Spika Ndugai baada ya Sugu kuuliza amesema kuwa “Mfano mzuri sana huo Mh. Sugu anatetea Jeshi la Magereza, Mh. Waziri unasemaje,” alisema Spika Ndugai.

Kwa upande wake Waziri Mwigulu amesema kuwa “Nimpongeze Mh. Sugu kwa kuuliza swali kwa experience na niseme tu kwamba yeye ni mshauri mzuri tutazingatia hilo ili tuweke mgao kwenye upande wa Jeshi la Magereza ili kuepuka tahadhari hiyo aliyoisema.”

Story ::   
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment