“Mimi vision yangu ni kuwa mfanyabiashara, sina ndoto ya kuimba milele'' Diamond Platnumz

Diamond anaangalia sana maisha yake ya mbele na anajiona kua mfanyabiashara zaidi kuliko Mwanamuziki.Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amesema kuwa anajua hawezi kuimba kwa kipindi chote hivyo mipango yake kwa siku zijazo ni kuwa mfanyabiashara.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kipindi cha Nyumba ya Imani kitakachokuwa kikiruka Wasafi TV, Diamond amesema kuwa anatumia muziki kama sehemu ya kujipatia mtaji tu.
“Kazi tunayoifanya sio kwamba Mwenyenzi Mungu anaipenda, kiuhalali haipo hivyo, hivyo tujitahidi kutenda matendo mengi mazuri, tutumie muziki katika njia nzuri,” amesema.
“Mimi vision yangu ni kuwa mfanyabiashara, sina ndoto ya kuimba milele, huwezi kuimba milele, kwa hiyo natumia muziki kesho na keshokutwa iwe ni chanzo cha biashara zangu nyingine na namshukuru Mwenyenzi Mungu siku zinavyozidi kwenda anazidi kunibariki,” amesisitiza.
Diamond tayari ameshaonyesha mwanga kwa upande wa biashara kwa kuachia sokoni bidhaa kama Diamond Karanga, Chibu Perfume na sasa Wasafi Media
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment