Uvaaji wa Kanzu na Hijab kipindi hiki cha Ramadan Kimemfurahisha Spika Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wabunge kwa kuvaa Kanzu kwa wingi na kwa Wabunge wa Kike kuvaa Hijab.

Spika ametoa pongezi hizo leo, Mei 18 mapema katikati ya kipindi cha maswali na Majibu kwa serikali likiendelea Jijini Dodoma ambapo pia amemsifia Naibu Spika wa Bunge kwa kuvaa Baibui na Hijab.

Naibu Spika, Tulia Ackson akiwa ndani ya Baibui leo
“Wabunge leo naona mnang’aa kwa kuvaa Kanzu, kiukweli mmependeza sana, lakini mkivaa inabidi mvae kama watu wa Pwani msivae viatu vya kamba ila mvae kobazi, lakini hata wabunge wa kike mmependeza naona Hijab nyingi lakini ya Naibu Spika wangu ni nzuri pia hii inaonyesha kuwa Tanzania ni wamoja,” amesema Spika Ndugai.
Source ;Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment