Zitto kabwe akumbuka Bunge la Tisa Baada ya Sakata la Mafuta na Sukari Kutikisa Bunge

Pale kitu kizuri kinapofanyika na kuonekane ni vyema kisemwe vizuri ,Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai baada ya kusimamia suala la kupanda kwa bei na kuitaka serikali itoe majibu ya kina kuhusu kupanda bei ya sukari ,akaitaka Serikali ije na majibu sahihi na ya kueleweka sababu Bunge sio sehem ya kubangaiza.

Zitto ametaka na suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa wakulima wa Mawese na Alizeti.
“Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la Majibu ya Serikali kuhusu Kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha Bunge la Tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka ‘legacy’ yake. Aendelee hivi. MUHIMU: Suala la Mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti,” ameandika Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo jana, Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alishindwa kutoa majibu ya serikali baada ya Mbunge wa Mpendae, Salim Turky (CCM), kuihoji serikali, Kwanini sukari imekuwa ikiuzwa bei ghali upande wa Tanzania Bara tofauti na ilivyo Zanzibar.
Jana, Spika Ndugai aliingilia kati suala hilo la kupanda kwa bei ya sukari na kusema kuwa “suala hili ni la Msingi sana kwa wananchi wa Tanzania na kwakweli halijapata majibu kwahiyo tutalipanga tena kwenye maswali ya wiki ijayo ili serikali itupe majibu ya kina linapaswa kutolewa majibu ya kina na serikali.”
story::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment