Naibu Spika Tulia Ackson alivyomkataza Waziri Mkuu kujibu swali linalohusu Waraka KKKT

Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson amemzuia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kujibu swali aliloulizwa na Mbunge Vunjo, James Mbatiakuhusu agizo la Serikali kwa Kanisa la Kilutheri kufuta waraka wake.

Naibu Spika alitoa zuio hilo kwa Waziri Mkuu huku akitumia mfano kuwa Spika wa Bunge alishawahi kumzuia Mbunge Saed Kubenea kujibiwa maswali yake yanayohusu dini.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia alitaka kujua Serikali inatoa tamko gani juu ya nyaraka hizo ambazo zimezua taharuki kwa jamii hasa ukizingatia Makanisa ni wadau wakubwa wa amani na maendeleo katika jamii.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment