Rais Magufuli atoa Maagizo Haya akizindua Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II). Nakusogezea Maagizo 12 aliyoyatoa Rais na mambo mengine aliyozungumza.

“Nimpongeze Waziri Mkuu wa Zamani Mizengo Pinda, katika awamu yake alizungumzia kilimo kwanza, akaishia yeye kwenda kuwinda asali kule Dodoma. Na huu ni mfano mkubwa kwetu sisi kwamba kilimo ni pamoja na ufugaji” -Rais Magufuli
“Kufukuza sio kitu kizuri lakini kuna wakati unatakiwa ufanye hivyo kama mtu anashindwa kutimiza majukumu, nampa mtu mmoja adhabu kwa faida ya watu Milioni. Watendaji wa serikali msiogope kufukuza” Rais Magufuli
“Nawakumbusha Mabalozi wa Tanzania walioko nje kuwa moja ya majukumu yao ni kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zetu za kilimo”-Rais Magufuli
“Chuo Kikuu Sokoine kifanye tafiti nyingi za kilimo na kubuni teknolojia za kisasa, pia kianzishe mashamba ya mifano kote nchini”-Rais Magufuli
“Natoa wito kwa REA na TARURA kuongeza kasi katika ujenzi wa barabara na usambazaji umeme vijijini ili kurahisisha uzalishaji na usafirishaji”-Rais Magufuli
“Naomba niseme ukweli, sijaridhika na utendaji kazi wa Benki ya Kilimo, ilianzishwa mwaka 2014 lakini inatoa mikopo kwa kusuasua na sifahamu kama Mkuregenzi wa benki hiyo kama anafanya kazi – Rais Magufuli
“Kuna siku nilikuwa naangalia habari, nikaona Naibu Waziri Kilimo ameenda kukagua ghala la korosho akakuta limejengwa kwenye mto wakati korosho haihitaji unyevu, limejengwa kwa zaidi ya Bilioni 5. Nilimwambia Waziri wa Kilimo afukuze wahusika” -JPM
“Matumizi ya mbinu duni za kilimo yanachangia kufeli kwa sekta ya kilimo kwani takribani asilimia 90 ya wakulima wetu bado wanategemea jembe la mkono na wanategemea mvua” -Rais Magufuli
“Sekta ya kilimo hivi sasa inachangia zaidi ya Asilimia 100 ya mahitaji ya chakula nchini, asilimia 30 ya pato la Taifa. Toka 2016 tumekuwa na ziada ya uzalishaji wa chakula. Haya ni mafanikio makubwa” – Rais Magufuli
“Sekta ya kilimo ni muhimu katika kuleta maendeleo, nchi zilizoendelea zimetufundisha mageuzi katika sekta ya kilomo ni kichocheo muhimu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi” -Rais Magufuli
“Ninawashangaa wanaosema hatupeleki fedha katika sekta ya kilimo ukweli ni kwamba tunapeleka ila inawezekana hazitoshi”, – Rais Magufuli
“Ninaamini kuwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu hayategemei itikadi za nyama, dini wala kabila” Rais Magufuli.
source ;;millardayo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment