Wakurugenzi Jamii Forums waachiwa huru na Mahakama

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa mtandao huo,Micke William kwa sababu hawana kesi ya kujibu.

Viongozi hao, wameachiwa huru na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 6 wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi uĺiotolewa una mashaka na kwamba hauna mashiko.
“Nawaachia huru washtakiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa hauna mashiko,”amesema Mwambapa
Katika kesi hiyo inayowakabili Melo na mwenzie wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi.
Source::millardayo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment