Aliyekua Mchumba wa Nay wa Mitego Nini Asema ameachana na Nay kisa ana wanaweake wengi

Kuna kipindi walikiki sana Nini na Nay wa mitego but wameshindwa kufikia happily ever after baada ya Nini kumwaga Nay wa Mitego kisa mashori wengi.

Muimbaji huyo alithibitisha kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM kwamba ni kweli alikuwa anatoka kimapenzi na rapa huyo ambaye alishirikiana naye kwenye wimbo, ‘Niwe Dawa’.
“Nay ana wanawake wengi sana, nimevumilia nikaona basi kila mtu achukue hamsini zake,” Nini aliuambia mtandao wa Samisago “Nimeshamsikiliza zaidi ya mara mbili lakini naona habadiliki nikaona bora kukaa pembeni,”
Muimbaji huyo amedai kuachana kwake na rapa huyo sio mwisho wa muziki wake kwani anajipanga upya na kuja kivingine.
Nay bado hajazungumza chochote kuhusiana na ishu hizo kwani kili akitafutwa kupitia simu yake ya mkononi hapatikani.
credit::bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment