Baada ya Shilole Kusema Muna ana roho ngumu,Joti na Irene Paul wamezungumza ishu ya Muna

Wiki mbili zimepita tokea muigizaji Munalove ampumzishe mwanae  Patrick katika nyumba yake ya milele na hivyo leo July 18,2018 kwa mara ya kwanza amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mwanae pamoja na baba mzazi wa Marehemu Patrick.

Muna Love kazungumza kile alichokiita ndo ukweli wa moyo kuhusu Baba wa marehemu mtoto wake na ishu nzima ya mazishi ilivyokuwa, Mchekeshaji Joti pamoja na Muigizaji Irene Paul wamezungumza kuhusu ishu hiyo ikiwemo suala la Shilole ambaye ameonesha kutofurahishwa na ishu hiyo ya Muna.Baada ya Muna kuongea na waandishi wa Habari ,Shilole alimchana muna love kwa kusema  hajawahi ona mwanamke mwenye roho ngumu kama Muna
Kupitia ukurasa wa instagram wa Shilole ameonyeshwa kuchukizwa na kitendo alichokifanya Munalove cha kuita na kuzungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa hajawahi kuona mwanamke kama Muna
“Hakuna siku nimevurugwa kama Leo, hakuna mwanamke wa namna hii kwenye hii Dunia!!! Sijawahi kuona mwanamke mwenye roho ngumu kwenye hii Dunia kama munah!!..😢😢😢😢#YouGirlUtapataTabuSanaaaa!!!”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.