Baraza la Taifa la Usalama barabarani Lavunjwa na Waziri Lugola

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelivunja rasmi Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na mabaraza yote ya ngazi ya mkoa akiwa jijini Mbeya.


Kangi amesema kuwa kuanzia leo anavunja Baraza hilo na ataunda upya ili kuokoa maisha ya wananchi kwa ajali za barabarani.
“Kwa mamlaka niliyo nayo kwenye sheria niliyoisema kuanzia sasa muda huu ninavunja rasmi Baraza la Usalama Barabarani la Taifa, nakuanzia sasa navunja kamati zote za Usalama Barabarani za Mikoa yote na Wilaya na nitaziunda upya ili kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kuokoa tunaokoa maisha ya wenzetu, Siwezi kuwa Waziri ambaye Rais wangu aliyeniteua anakerwa na mambo haya haiwezekani hilo la kwanza,” amesema Kangi Lugola.
Julai 01, 2018, Rais Dkt John Magufuli alimteua Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba, huku akimtaka waziri huyo mpya kushughulikia sakata la Lugumi, ajali, sare za polisi, uingizwaji wa mizigo bandarini na mambo mengine ya usalama wa nchi.
credit::bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment