Faiza Ally Awashutumu mashabiki Instagram ndio husababisha watu wawe na maisha feki sababu wanayashabikia

Kuna msemo unasema penye watu wengi daima hapawezi kukosa maneno na hivyo ndivyo ilivyo kwenye mitandao ya kijamii na hii ni baada ya Faiza Ally kupost kuhusiana na mashabiki wa instagram na kuwaona ni wachochezi kwa watu na kuwafanya waishi maisha feki ambayo hayana uasilia wa kweli.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Faiza Ally amewashtumu mashabiki kuwa wanayumbisha maisha ya watu na kuwafanya waishi maisha feki kutokana na wengi kuongelewa vibaya na hivyo inahitaji mtu jasiri kuonyesha uasilia halisi wa maisha yake.
“Nyie mashabiki wa insta mnayumbisha akili za watu ndio maana mnafanya watu waishi maisha feki …it takes very strong person kuishi maisha yake halisi …maana watu halisi mnawebeza mnashabikia feki na sasa ili waendelee kujisikia vizuri inabidi waendelee kufeki hata kama wanapita juu ya miba wawape furaha huku wanakufa na tai shingoni ! Feki + feki + feki sawasawa na zero”Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment