Huko Uholanzi Watoto wafariki baaa ya wajawazito kupewa dawa ya kuongeza nguvu za kiume

Utafiti wa wanawake wajawazito umesitishwa mara moja baada ya watoto wachanga 11 kuaga dunia.
Wanawake waliokuwa wakishiriki katika utafiti huo wa Uholanzi walikuwa wamepatiwa dawa ya viagra ili kuimarisha ukuwaji miongoni mwa watoto ambao hawajazaliwa kwasababu walikuwa na kondo la nyuma ambalo halikuimarika.
Inaonekana kwamba dawa hiyo, inayoimarisha usambazaji wa damu katika mwili huenda iliharibu pakubwa mapafu ya watoto hao.
Wataalam wanasema kuwa uchunguzi kamili unahitajika kuelewa kilichofanyika. Hakuna madai yoyote kwamba kulikuwa na makosa yoyote.

Watoto wagonjwa

Vipimo vya awali vilivyofanyika nchini Uingereza na Australia pamoja na New Zealand havikuonyesha ushahidi wowote mpya baada ya hatua hiyo. Lakini pia ulisaidia.
Wakati huo, 2010, watafiti walisema kuwa tiba hiyo inafaa kutumika kwa majaribio pekee.
Ukuwaji wa mtoto aliye tumboni unaozuiwa na kondo la nyuma lisilokuwa ni hali mbaya ambayo haina dawa.
Inamaanisha kwamba watoto huzaliwa kabla ya kukomaa, wakiwa na uzani mdogo na fursa chache za kuishi.
Dawa inayoweza kuimarisha uzani ama hata kuongeza muda wa kujifungua inaweza kutoa fursa nzuri kwa watoto hao wagonjwa.
Utafiti huo wa Uholanzi ambao ungeendelea kufanyika hadi 2020 ulikuwa ukifanywa katika hospitali 11 nchini humo ikiwemo chuo kikuu cha matibabu cha Amsterdam.
Kwa jumla ,wanawake 93 walipatiwa sildenafil (Jina jengine la Vagra) hukiu waliosalia 90 wakipewa dawa kama hiyo au Placebo.
Watoto 20 walikumbwa na matatizo ya mapafu baada ya kuzaliwa -watatu katika kundi la Placebo na waliosalia katika kundi la matibabu.
Watoto 11 kutoka kundi la Placebo walifariki kutokana na matatizo ya mapafu.
Profesa Zarcko Alfirevic, kutoka chuo kikuu cha Liverpool, ambaye aliongoza utafiti miongoni mwa wajawazito uliobaini kwamba dawa hiyo haina usaidizi wowote katika ukuwaji wa mtoto ,alisema: Matokeo ya utafiti huu hayakutarajiwa.
''Tunahitaji kuwa makini zaidi wakati huu ili kubaini zaidi''.
"Unahitaji uchunguzi wa kina kwasababu athari zake hazikuonekana katika vipimo vyengine viwili , ikiwa ni vipimo sawa na vile vilivyofanyika nchini Uingereza, Australia na New Zealand
BBC Swahili
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.