Lazaro Nyalandu Atoa Majibu baada ya kuambiwa arudishe Twiga

aziri wa zamani wa Maliasili na Utalii kwenye Serikali ya awamu ya nne Tanzania Lazaro Nyalandu ameingia tena kwenye headline, wakati huu ni baada ya kuambiwa arudishe Twiga.

Ilianzia pale Nyalandu alipoandika maneno ya kutia moyo >>> “Ukweli katika maisha ni huu, kwamba MUNGU hakuachi. Amini katika UWEZO na UKUU wake. Ujapopita katika changamoto zozote katika MAISHA, hata wale wa karibu nawe wakikuacha, Yeye ni AMINI na KWELI, HATAKUACHA, atakupigania, na atakufanya HERI kwa ajili ya UTUKUFU wake. 
Baada ya kuandika maneno hayo mmoja wa Followers kwenye mtandao huo wa Twitter alimjibu kwa kuandika “Ukirudisha Twiga tutakuelewa” ndipo Nyalandu akamjibu kama inavyosomeka hapa chini.
“Watu kama wewe wamelaaniwa. Huwezi kuanza siku kwa kusema UONGO ili ujisikie umesomeka kwenye mitandao ya kijamii. Ni TWIGA yupi unayetaka nimrudishe, na nilimchukua WAPI. Imeandikwa, WAONGO wote, sehemu yao ni katika ZIWA liwakalo kwa KIBERITI” – Nyalandu

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.