Maamuzi ya Waziri Jafo baada ya Jangwani Sekondari kuwa ya mwisho

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ametembelea Shule ya Jangwani Sekondari Dar es salaam ambayo imetajwa juzi kuwa miongoni mwa Shule 10 zilizoshika nafasi za mwisho katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.


Jafo amesema Shule hiyo ni miongoni mwa Shule chache zenye Walimu wengi lakini imekuwa katika kundi la mwisho “Shule ya Jangwani ina walimu 87, Shule ya Kibaha ina Walimu 52, yenye Walimu 52 inakua ya kwanza kitaifa lakini yenye Walimu 87 inakua ya tatu kutoka mwisho kitaifa”

Waziri Jafo ametoa maagizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa Afisa wa DSM abadilishe uongozi lakini pia mabadiliko ya Walimu yafanyike.

“Badilisheni Walimu wa Jangwani, waleteni Walimu wengine waje wafanye mabadiliko hapa, nimepata taarifa kuwa kuna Walimu hawafundishi, watoto wanajipinda wanaandika notes wenyewe, wengine wana moyo wa kusoma lakini Walimu wenye moyo hakuna,”

Mrembo Jokate akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Jangwani katika project zake za Netball. Picha hii sio ya tukio la hivi karibuni
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo jana Julai 17, 2018 wakati alipokuwa shuleni hapo na kumuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa shule hiyo kwa kuwa hajaridhishwa na ufaulu wa wanafunzi kwa sababu Jangwani ndio shule ya ndoto ya wasichana wengi wa kitanzania.
“Shule ya Jangwani ni shule ambayo yenye upako maalum, sifa na tunu kwa nchi yetu lakini shule hii sasa imekuwa ya tatu kutoka mwisho. Hii ni fedheha ambayo haijawahi kutokea katika shule ya Jangwani. Wanafunzi mmekuja hapa kwaajili ya kusoma sio kwa sketi zenu za rangi ya chungwa, tunataka msome…..
Kwa taarifa nilizozipata wanafunzi wanatumia simu hizi za Whatsapp na muda mwingi wanaangalia picha zilizokuwa mbovu badala ya kusoma huku wengine wakikalia ku-chat na kuangalia vitu ambavyo sio sawa sawa”, amesema Jafo.
Pamoja na hayo, Jafo ameendelea kwa kusema “kwa taarifa nilizozipata hapa za kiuchunguzi ni kwamba wanafunzi wengi wanajihusisha na mambo ya uhasharati, naomba niwaambie endapo mtajihusisha na mambo hayo, elimu haitaweza kuwa rafiki yenu na hilo jambo hata wakubwa wazima linawashughulisha sembuse nyie wanafunzi, nasema kuanzia leo hilo suala lishindwe na ndio maana ufaulu wenu unakuwa mbovu”.
Shule hiyo kongwe iliyopo eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam imeingia kwenye nafasi ya 10 shule zilizoweza kufanya vibaya katika matokeo yaliyotangazwa Julai 13, 2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).
Shule 10 za mwisho kitaifa ni Jangwani ya mkoani Dar es Salaam, Jang’ombe (Mjini Magharibi), Forest Hill (Morogoro), St James Kilolo (Iringa), Aggrey (Mbeya), Nyailigamba (Kagera), White Lake (Dar es Salaam), Musoma Utalii (Mara), Golden Ridge (Geita) na Ben Bella (Mjini Magharibi).
Huku shule 10 zilizoweza kufanya vizuri zaidi zikiwa ni Kibaha ya Mkoani Pwani, Kisimiri (Arusha), Kemebos (Kagera), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys’ (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Ahmes (Pwani), St, Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Marian Girls (Pwani) pamoja na Feza Girls ya Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.