Watanzania Wanaoenda Kufanya Kazi Nchi za Nje Wabanwa na Lugola

: Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Kamishna wa Uhamiaji kutotoa kibali kwa Mtanzania yeyote kuondoka nchini kwa madai ya kupata kazi nje ya nchi bila kujiridhisha kuwa anayo mikataba ya sehemu anayokwenda kufanya kazi


Amemtaka pia Kamishna wa Uhamiajia ajiridhishe kwa kufanya mawasiliano na Balozi husika katika nchi ambayo mtanzania huyo atadai anaenda kufanya kazi

Kauli hiyo ameitoa wakati wa shughuli ya maadhimisho ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu nchini jana Julai 30 katika viwanja vya Mnazi Mmoja

Pia amesisitiza kuwa Serikali haikatazi Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi bali kinachotakiwa ni kufuata utaratibu kutokana na nchi kuendelea kuathirika na watu kusafirishwa kiharamu na kwenda kuteswa

Aidha, Waziri Lugola ameagiza msako wa nyumba kwa nyumba, mashamba kwa mashamba, viwanda kwa viwanda na sehemu zote zinazotoa ajira kuangalia kama kuna Wahamiaji haramu walioajiriwa

Katika hatua nyingine kwenye maadhimisho hayo, Waziri Lugola amemfuta kazi Mjumbe wa Sekretarieti ya kupinga usafirishaji Haramu wa binadamu kwa kushindwa kujua idadi ya vyombo vinavyotakiwa kutaifishwa 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.