Wema amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au faini Mil. 2

Muigizaji Staa na Miss Tanzania 2016 Wema Sepetu amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Tsh. Milioni mbili baada ya kukutwa na hatia ya kukutwa na kutumia Dawa za Kulevya.

Wema amekutwa na hatia katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Thomas Simba leo katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.
Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.
Katika hukumu nyingine wafanyakazi wawili wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.