Hongera kwa Mwanamuziki A.y na Mke wake kwakupa tamtoto wa Kiume

Staa wa muziki wa Bongofleva Ambewne Yesaya “AY”,alitumia mtandao wa instagram kutoa habari njema kwa mashabiki wake kwamba yeye pamoja na mkewe Remmy wamemkaribisha mtoto wao wa kwanza wa kiume katika familia yao.

AY ametangaza rasmi kwa mashabiki wake kuwa amefanikiwa kupata mtoto wa kiume aliyezaliwa siku ya Jumapili ya August 12 2018 katika mji wa Dallas Texas Marekani katika hospitali ya Medical City Healthcare.
Kupitia ukurasa wa instagram wa AY ameandika ujumbe mfupi ku’share good news hizo na mashabiki wake na tayari mtoto huyo ameshapewa jina la Aviel likiwa na maana ya“Mungu ndio baba yangu”

“Mungu ni Mwema na namshukuru sana kwa kutubariki mimi na My Beautiful Wife #Remytarehe 12.08.2018 Medical City Healthcare Dallas -Texas tumepata mtoto wa kiume AVIEL maana yake GOD IS MY FATHER…. 3.9Kgs & 27 inches…Welcome to the World AVIEL YESSAYAH 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment