Ili Joh Makini aache Muziki labda kifo kiwatenganishe lakini si vinginevyo

HAPPY BELATED BIRTHDAY MWAMBA WA KASKAZINI ,JOH MAKINI

Tarehe 27 mwezi 8 ilikua siku ya kuzaliwa kwa Rapper maarufu Bongo na nje ya mipaka yake Joh Makini alipata fursa katika kituo cha redio cha East Africa Radio na kufunguka kama aliwahi kufikiria kuacha muziki na kufanya ishu zingine.

Joh amedai haitokuja kutokea maishani mwake, kuacha kurap labda kifo ndio kiwe sababu ya yeye kumtenganisha na muziki.
“Kufanya vitu vingine tofauti katika maisha hilo ni muhimu kabisa, lakini kufikiria kuacha muziki sijui, kwasababu na kuwa mzito sana kusema itafikia siku ntashindwa kurap ?, sijui ila napenda muziki sana”, amesema Joh Makini.
Aliongeza “Endapo ikitokea nikiacha kurap na kutoenda studio lazima ntakuwa kwenye mzunguko wa kufanya vitu vingine na muziki pia. Sioni sababu ya kuacha muziki labda kifo ndio kitanitenganisha lakini sio kitu kingine”.
Wasanii wengi wanakuwa kwenye wakati mgumu pindi wanapoulizwa kuhusu kuachana na muziki, kutokana na baadhi yao kufanya muziki kama kazi na starehe hivyo kuwawia vugumu kuachana na vitu hivyo kutokana na mazoea.
Mbali na hilo, Joh Makini amesema kwa sasa muziki wa hiphop nchini unalipa kwa kiasi kikubwa, tofauti na ulivyokuwa zamani huku akiwarushia dongo wasanii wanaolalamikia kuwa yawezekana wao wenyewe hawajajipanga katika kutoa kazi nzuri ndio maana wanayumba.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment