Julius Malema Kiongozi wa Upinzani Africa kusini Asema African iungane na Itumie Lugha ya Kiswahili

Kiongozi mkubwa nchini Afrika Kusini wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema, amependekeza bara la Afrika Liungane na liwe na sarafu yake kama ilivyo Ulaya na kutumia lugha moja ya kiswahili ili kuepuka lugha za kikoloni ambazo zinatumiwa kututenganisha.

Malema amesema hayo jana Agosti 29, 2018 kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na EFF kama sherehe ya miaka mitano tangu chama hicho kianzishwe, ambapo aliongelewa mambo mbalimbali ikiwemo ujumbe wa Rais wa Marekani kwenye mtandao wa Twitter kuhusu marekebisho ya sheria ya ardhi Afrika Kusini ambapo amesema bara la Afrika haliwezi kukubaliana na mtu kama huyo anayeona watu weupe wananyanyaswa.
Lazima tukuze lugha moja ambayo itatumika kwenye bara zima. Madharani Kiswahili, kinaweza kukuzwa ili kitumike bara zima la Afrika,” amesema Malema.
Kwa upande mwingine Malema amesema kuwa ni vyema wazo la Marehemu Ghadafi la kuunganisha bara la Afrika lifufuliwe ili iwe rahisi kuwa na sarafu moja na hatimaye kuepukana na ukoloni mamboleo.
Akikazia kuhusu lugha za kigeni, Malema amesema lugha kama kifaransa, Kiingereza na Kireno zililetwa kutuchonganisha na kututenganisha ili tusiungane, kiurahisi hivyo haoni umuhimu wa lugha hizo kuendelea kusalia barani Afrika.
Hata hivyo amewaonya wanawake wa Afrika kuacha mara moja kuvaa mawigi kwani ni moja ya njia ya kuendeleza ukoloni, huku akidai kuwa Kenya ni taifa ambalo halijapata uhuru kamili kwani ni vibaraka wakubwa wa mataifa ya Ulaya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment