Rais Museven awasili Tanzania kwa Ziara ya Siku Moja

Rais wa Uganda, Yoweri Museven amewasili Tanzania kwa ziara ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli kisha wawili hao kuongozana hadi Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Museven amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa 3:45 asubuhi ya leo kisha kupokelewa kwa ngoma za asili na kusalimiana na maofisa wa Serikali wa hapa nchini.
Viongozi hao watakuwa na majadiliano ya faragha Ikulu jijini Dar es salaam kisha kuzungumza na waandishi wa habari kabla Rais huyo wa Uganda hajarejea nyumbani.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.