Sumu ndiyo Chanzo cha Ugonjwa wa Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Yanje’ Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amedai sumu ndio chanzo cha ugonjwa wake.


Miezi michache iliyopita Ommy Dimpoz aliuambia uma wa Watanzania kuwa alikuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji ambapo chanzo kilikuwa ni ugonjwa Kwenye koo.

Baada ya taarifa za Ommy Dimpoz kuzidiwa ICU kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii siku chache zilizopita hatimaye mwenyewe amefunguka na kuweka wazi kuwa anaendelea vyema.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo huko Johannesburg South Africa ambako anaendelea na matibabu, Ommy ameweka wazi kuwa alienda Kwenye hospitali nchini Kenya na nchini South Africa na kote madaktari walimwambia kuwa aliwekewa sumu.

Ommy Dimpoz amedai alishangazwa sana alipoulizwa kama ameshawahi kunywa sumu kwani hajawahi kufanya hivyo kwa hiari yake Lakini pia amekataa kusema kama inawezekana aliwekewa sumu hiyo bila kujitambua.

Ommy ambaye anaonekana kupungua sana mwili amedai baada ya kuonekana na matatizo Kwenye koo yaliyokuwa yanamzuia Kula wala kunywa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kutengeneza njia mpya ya kupitisha chakula.

Ommy amesema anaendelea na matibabu nchini humo lakini ameweka wazi kuwa anashukuru Mungu kwani anaendelea vizuri sana kwa sasa tofauti na siku za nyuma. 
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment