Baba Diamond Amuomba Mwanae Ampe Mtaji wa kuuza Mitumba

Baba mzazi wa msanii Diamond Platinumz, Nzee Abdul ametuma salamu kwa mtoto wake na kuomba amsaidie kumpatia mtaji wa kuweza kufunfua duka kubwa ambalo litakuwa likimuingizia kipato ili aweze kumudu maisha yake.


Akitaja kuwa hata kama itakuwa duka la mitumba kwake itakuwa sawa kwa sababu hiyo ni moja ya biashara aliyoizoea tangu ujanani , lakini pia akiwa na uwezo basi anaweza kumfungulia duka kubwa lolote ili aweze kufanya kazi akiwa amepumzika bila mikiki mikiki yoyote.

Akiongea na waandishi wa habari, baba huyo amasema kuwa Diamond asifikirie kumnunuli gari kwa sababu gari hana uweoz nalo hata kidogo na ni kwa sababu gari inahitaji sana pesa kwa ajili ya kununua spare pale zinapoharibika lakini akimpa mtaji wa kufanya kitu gari atakuja kununua hata baadae akishauza mazao yake shambani.

Baba Diamond anasema kuwa asimpe gari kwa sababu atakaposhindwa kulihudumia , litamshinda na ataliweka uani lakii mwisho wa siku ataliuza kwa bei ndogo na ya hasara.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment