Mwanamuziki Shaa Aukacha Mziki na Kukimbilia Kilimo

Mtayarishaji wa Muziki maarufu na Mkongwe Katika tasnia ya Bongo fleva Master J ameweka wazi kuwa msanii wa Bongo fleva Sarah Kaisi maarufu kama Shaa ameachana na Mziki na kugeukia kilimo.

Master J ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Shaa kwa miaka mingi amesema ukimya wa Shaa Kwenye muziki ni kutokana na maamuziki ya kuweka sanaa pembeni.


Kwenye mahojiano na Bongo 5, Master J amedai Shaa ameamua kuacha muziki na kufanya kilimo kinachomuingizia kipato kikubwa zaidi na sasa yupo mkoani Mbeya.

Shaa ni mfanyabiashara sasa hivi yupo busy na kulima kule Mbeya naona inalipa zaidi nimejaribu kumshawishi arudi Kwenye muziki lakini ananiambia subiri apige kazi apate pesa ndio atarudi tena kwenye  muziki”.

Lakini pia Master J ameweka wazi kuwa yeye na Shaa bado wapo wote Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment