Ndoto ya Mfanyabiashara:: Nandy kuhusu kuacha kufanya muziki na Kusimamia Biashara zake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy amefunguka mwanzo mwisho kuhusu malengo yake ya kuachana na mziki na kuhamishia nguvu zake kwenye biashara.

Nandy ameongea hayo leo katika kituo cha habari cha Clouds Fm kwenye kipindi cha Leo tena na kusema  kuwa Bado miaka mitatu kuachana na muziki ” Mimi katika ndoto zangu ni kuwa mfanya biashara mkubwa sana na hata naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano nitaacha muziki na niendeleze biashara zangu na hadi sasa nimeitumia miaka miwili tu 2016,na 2017 na mwaka 2020 ndio nitaacha muziki na sio kuwa nitakuwa sitoi ngoma hapana nitakuwa natoa ila kwa mwaka hata mara moja pia kuhusu show naweza kuwa nafanya kwa mwaka mara moja ili nipate muda wa kusimamia baishara zangu”
Nandy ni kati ya wanamuziki wa kike kutoka Tanzania wanao fanya vizuri kwa sasa akitambulishwa na ngoma yake ya Ninogeshe.
Credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment