''Ninakikomo cha Mauvu Ila kwa Hili Kitakachokupata Nisilaumiwe"Kauli ya Zitto Kabwe kwa Cyprian Musiba

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe leo ameonekana kukerwa na Habari iliyochapishwa katika gazeti la Tanzanite ambalo linamilikiwa na  Cyprian Musiba ambalo limeandika story ya kumchafua katika ukrasa wa mbele (Front Page) kwa story iliyosomeka

Katika ukrasa wake wa instagram zitto Kabwe ameandika maneno makari na kumpa siku moja  Musiba na genge lake  kuthibitisha au kukanusha Habari yake ambayo wameitoa leo la sivyo akienda kinyume na hilo asilaumiwe.

"‪Deo alikuwa zaidi ya rafiki yangu. Kwangu mimi hajafa. Uzushi wa Gazeti la Tanzanite, kama ulilenga kuniumiza, wamefanikiwa sana. Ni tangazo la vita. Bahati mbaya sana hata mtu anayeamini chembe ya uzushi ule namwona adui ( mniwie radhi ). Cyprian Musiba na yeyote mwenye kuhusika na Gazeti la Tanzanite wanapaswa kupata funzo ambalo hawatasahau maishani. Sisi kwenye Siasa tunaweza kuvumilia mengi. Mimi kama Zitto nina kikomo cha uvumilivu. Ndugu wa Musiba na genge lake wasinilaumu kitakachompata ndugu yao. Ana siku moja tu kuthibitisha au kukanusha Habari yake ya leo. Baada ya kesho sitasikia rai ya Mtu yeyote. Inshallah Mwenyezi Mungu aendelee kunipa subra na hekima"
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment