Tuhuma za Uganga :: Diamond Ajibu Tuhuma za Kutaka Kulogwa na Hamissa Mobetto

Msanii Diamond Platnumz amejibu kuhusu voice note inayosambaa mtandaoni ambayo inadaiwa kuwa ni ya Hamisa Mobetto akipanga njama za kumloga muimbaji huyo pamoja na mama yake mzazi.

Sasa Diamond amesema kuwa anauhakika sauti hiyo ni ya Hamisa na kueleza kushangazwa kwake na kitendo hicho.

 “Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe,” alisema Diamond kupitia Refresh ya Wasafi TV.

Aliongeza,”Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi,”

Wiki hii dada wa Diamond Platnumz, Esma aliandika ujumbe mrefu kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kwamba wameandaa voice note kwaajili ya kumchafua Hamisa Mobetto.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment