Tweet ya Madee Kwa Waziri Dr Harrison Mwakyembe ''Ngoma Zetu Hazionekanai Kwenye Television za Nyumbani Chezesha Baba”

Msanii Madee kutokea kwenye industry ya Bong
o Fleva ameonekana kusikitishwa na asilimia kubwa ya vyombo vya habari kucheza ngoma za nchi za nje kuliko ngoma za wasanii wa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Madee amemuomba Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe kuliangalia swala hilo huku wengi wakiamini kuwa linashusha hadhi ya muziki wa Bongofleva pia inawakatisha tamaa wasanii.

Madee ameandika “Mh Waziri wa habari na Utamaduni baba yetu Harrison Mwakyembe ngoma zetu hazionekanai kwenye television za nyumbani tunaangalia mangoma ya nje tu yanayopigwa na television zao tafadhali chezesha baba”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment