Upasuaji:: Watoto walioungana sehemu ya INI wafanyiwa upasuaji Muhimbili

 Watoto wawili waliokuwa wameungana tumboni watenganishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambao walizaliwa katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mwaka huu July 12.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Prof. Laurence Moselu amesema upasuaji ulifanyika September 23 kwa mafanikio na kuwa watoto hao wanaendelea vizuri.
Amesema “Tulifikiri kwamba upasuaji huu ungekuwa mgumu lakini tumefanikisha na tuna vyumba viwili ya upasuji kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitatu jambo linalopunguza watoto kusubiri upasuaji kwa muda mrefu”
Aidha, Daktari bingwa wa upasuaji kwa watoto Dkt. Petronila Ngiloi amesema “Wakati watoto hao wanatenganishwa walikuwa na kilo 9, mmoja alikuwa na kilo 4 na mwingine kilo 5”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment