Habari Njema kwa Wasanii :::: BASATA kuthibiti maudhui ya nyimbo za wasanii kupitia WhatsApp

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limeanzisha utaratibu wa kukagua nyimbo za wasanii kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.
Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, amesema wamefikia hatua hiyo kama njia ya kuwarahisishia wasanii kukaguliwa kazi zao.
Sababu nyingine amesema ni kutokana na kukua kwa teknolojia wameona nao waendane sambamba na ulimwengu huo.
Mngereza alizitaja namba hizo kuwa ni 0783 965 337, ambapo msanii atatuma kazi yake na kupewa majibu haraka kama inafaa kwenda kwa jamii au la.
“Teknolojia imekuwa kubwa sana, hatuoni tena sababu ya kumsumbua msanii aje ofisi kwetu kwa ajili ya kukaguliwa nyimbo wakati kazi hiyo anaweza kuifanya hata akiwa nyumbani kwake.
“Pia, tunaamini itampunguzia gharama na kuokoa muda ambao atautumia kufanya mambo mengine, hivyo wale waliokuwa na visingizio ya hayo sasa hatufikirii tena kuvisikia kwani tumewarahisishia maisha ni wao wenyewe,” amesema Mngereza.
Akizungumzia hali ya wasanii kupeleka kazi zao kukaguliwa kabla ya kuzitoa, alisema kwa sasa uelewa umeongezeka kwa baadhi yao ambapo kwa siku wanaweza kupata hadi kazi 15 zinazotakiwa kukaguliwa.
credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment