Hii ndo Gari iliyomteka MO na mmiliki na dereva wanafahamika IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema mpaka sasa watu nane kati ya 27 bado wanashikiliwa na polisi kutokana na kutekwa Mohammed Dewji ‘Mo’ huku akidai hawajui kama bilionea huyo yupo hai.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, Sirri amedai mpaka sasa tayari wameweza kugundua gari ambayo inadaiwa kumteka mfanyabishara huyo.
“Swala la Mo yupo hai ama hayupo hai sina jibu,lengo ni kwanini ametekwa sina jibu wala gari imetoka nchi gani na dereva ni nani tutawaambia maana uchunguzi unaendelea” IGP Siro.
Kauli za IGP Sirro na waandishi.
“Tumeshatambua gari aliyotekwa na Mo.Gari alilotekwa Mo lilitokea nchi Jirani. Liliingia nchini Tarehe 1 sept 2018. Tunashirikiana na wenzetu Interpol, na tumeshamtambua dereva wa gari hilo,” Sirro
“Niwatumie salamu Hawa wahusika wa tukio hili. Hii ni siku ya tisa tunazunguka, watu wangu hawalali. Tukiwakamata watajua Hii ni Tanzania,” Sirro.
“Tumeshatambua gari aliyotekwa na Mo.Gari alilotekwa Mo lilitokea nchi Jirani. Liliingia nchini Tarehe 1 sept 2018. Tunashirikiana na wenzetu Interpol, na tumeshamtambua dereva wa gari hilo,” Sirro
credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment