Msimamo wa serikali kuhusu korosho watolewa na Raisi Magufuli

Rais John Magufuli ametoa msimamo wa serikali kuwa bei ya korosho isipungue Shilingi 3000 kwa kilo moja.

Rais Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Korosho.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 alipokutana na wadau na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
"Mimi nataka muende mkakae vikao vyenu huko mkubaliane, lakini bei ninayoitaka ni kuanzia sh 3000 na kupanda juu, na kama hamko tayari mniambie tu hapa sasa hivi nipange jeshi langu, nimeshaongea na Jenerali Mabeyo", amesema Rais Magufuli.
Hayo yamejiri baada ya wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuingia kwenye mgomo wa kuuza zao hilo la Korosho kwa kile walichokidai kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita huku gharama za uzalishaji zikiwa zimepanda.
Kufuatia mgomo wa minada ya siku mbili, Oktoba 26, Rais Magufuli, alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwaeleza kuwa anaunga mkono hatua ya maamuzi hayo ya wakulima na kusema yuko nao bega kwa bega.
Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na watendaji wengine wa serikali.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment