Mwanaharakati wa Haki za watoto na wanawake Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, pamoja na wenzake watatu wameshinda tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2018. Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Fernanda Espinosa, kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza kwa mchango wao wa kusongesha mbele haki za binadamu.
Kwa mujibu wa BBC, Rebeca na washindi wengine watatu wa mwaka huu watapatiwa tuzo yao mjini New York, Marekani tarehe 10 Desemba mwaka huu, wakati wa kilele cha tamko la haki za binadamu la umoja wa mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 70.
Mshindi mwingine ni Asma Jahangir mwanaharakati na mwanasheria wa Pakistani ambaye amefariki dunia mwaka huu.Tuzo hiyo ilianza kutolewa mnamo mwaka 1973 na hadi leo imetolewa mara 10.
“Kile tumekuwa tukikifanya ni kuwahamasisha wasichana kusimamia ndoto zao na kuzifikia katika jamii, kitu ambacho kimechukuliwa kuwa cha umuhimu,” “Kwetu ni furaha kuwa dunia imetambua kile tukifanya na sasa ni fursa muhimu kuzungumzia changamoto ambazo wasichana wanapitia, na kuihamasisha serikali na wadau kuweza kuona faida ya mtoto wa kike katika maendeleo ya jamii,” Bi Gyumi aliiambia BBC.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment