Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine wa Body ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua, Dkt Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC.

Awali Dkt Sophia Kongela alikuwa mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi nchini.
Aidha kupitia Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemteua Dkt Maulid Banyani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba la taifa.
Awali Dkt Banyani naye alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) nchini ambapo awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Felix Maagi
Mapema asubuhi ya leo, Oktoba 30, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alitangaza kumteua Prof. Humphrey Moshi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani nchini (The Fair Competition Commission- FCC).
Tangu aingie madarakani Rais John Pombe Magufuli amekuwa akiwateua wasomi mbalimbali kushika nafasi za uongozi kwenye mashirika ya umma, binafsi na kutoka vyama mbalimbali vya siasa
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment