Tweet ya Kwanza ya Mo Dewji kwa watanzania

Zikiwa ni siku ya tatu tangu kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji 'Mo Dewji', mfanyabiashara huyo ametoa neno la shukrani kwa mwenyezi Mungu na watanzania kwa kumuombea katika kipindi chote alichokuwa mateka.
Kupitia mtandao wake wa 'twitter' Mo Dewji ameandika kuwa, "Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu".
Mo Dewji ameongeza kuwa, "Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima".'

Mfanyabishara huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akielekea mazoezini na kuachiwa Alfajiri ya Oktoba 19, ambapo alikutwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment