Viwanda 73 kujengwa Pwani na Viwanja vya Mpira miguu

Wananchi wenye viwanja na maeneo makubwa nchini ambayo yanafaa kwa uwekezaji wameshauriwa kwenda katika kituo cha uwekezaji Tanzania TIC ili kuona ni kwa namna gani wataweza kuyatumia maeneo hayo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji kutoka katika Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Ayoub Sizya wakati akitembelea na kukagua eneo la ukanda wa uwekezaji na mauzo ya ndani na nje ya nchi la Kiluwa lililopo kijiji cha Disunyala Kata ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
“Sisi TIC  na Ukanda huu wa uwekezaji wa Kiluwa lengo letu ni kuimarisha shughuli za uwekezaji, tunafanya hivi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi, kama unavyojua eneo hili linamilikiwa na mtu binafsi, na ni eneo kubwa, hivyo tukiungana tutaleta wawekezaji wengi zaidi Tanzania ya Viwanda itazidi kusonga mbele” amesema Ayoub Sizya Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji TIC
Mmiliki wa eneo hilo la ukanda wa uwekezaji Mohammed Kiluwa amesema watajenga viwanda zaidi ya 70 na kwamba mpaka sasa kiwanda kimoja kimekamilika ujenzi wake huku vingine saba vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu viwanda 20 vitakuwa vimeanza ujenzi.
“Tutajenga viwanda vingi, ni zaidi ya 70 na kwenye eneo hili tayari tumepata maombi ya zaidi ya ujenzi wa viwanda 20 kwa mwaka huu, Tanzania ya Viwanda itafanikiwa tu, lengo letu ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli” alisema Mohammed Kilua Mkurugenzi wa eneo la ukanda wa uwekezaji la Kilua Mohammed Kilua.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment