DC wa Njombe aagiza vijana wanaovaa mlegezo ‘Kata-K’, vimini na nguo za kubana wachapwe viboko hadharani

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe, Veronika Kessy ametoa amri ya kupewa adhabu ya kuchapwa viboko kwa vijana au mtu yeyote atakaye onekana kuvaa mavazi yasiyo na staha katika jamii.
DC Kessy ametoa agizo hilo alipo kuwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kata za Iniho na Kipagalo wilayani humo,  ambapo amesema mavazi hayo sio maadili ya wakazi wa wilaya hiyo.
Akielezea adhabu hiyo,  DC Kessy amesema kuwa vijana wakiume wanaovaa suruali mlegezo (Kata-K) au wasichana wanaovaa mavazi yanayobana au yanayoonesha maumbile yao au mavazi yanayochora miili yao wachapwe viboko Kama adhabu mbadala.
”Nataka kuona vijana suruali zenu zinashuka kutokana na waleti kuwa nzito, umefanya shughuli zako huko waleti imejaa hela ndio inashusha sio kushusha tu ni viboko nasisitiza ni viboko wakati sheria za adhabu zingine zikiendelea kutungwa huko kwenye kata’,”amefunguka DC Kessy.
”Huu ni utamaduni wa wapi?? sie wabantu hatuna utamaduni huo naagiza mkimkamata chapa viboko tu,watoto wetu hao!”.
Kwa upande mwingine, DC kessy amemtaka mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete, Godfrey Gogadi kushirikiana na serikali za vijiji kutunga sheria itakayomhukumu na kupewa adhabu kwa watu wa aina hiyo.
credit::Bongo5
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment