ELIZABETH MICHAEL aka Lulu AMALIZA KIFUNGO CHAKE ,NA SASA YUKO HURU

Muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael aka Lulu sasa amemaliza kifungo chake na yuko huru.Alikua akitumikia kifungo hicho cha nje kwa muda wa saa akiwa nje na November 12 leo ndio anakua huru.Lulu alipangiwa kifungo cha nje akiwa anafanya kazi mbalimbali za kijamii.

Muigizaji Lulu alihukumiwa kifungo cha jela baada ya kukutwa na kesi ya kuua bila kukusudia kwa mwigizaji mwenzake Steven Kanumba ambae alikua mpenzi wake .
Dr.Cheni ambaye ni mwanafamilia wa Mwigizaji Lulu ametumia mtandao wa kijamii kutoa habari hizi na haya ndiyo aloandika.

Sina la kusema @elizabethmichaelofficial zaid ya kumshukuru Mungu na kumwambia Mungu Asantee Kwa hili jambo kuisha salama Unajuwa jinsi gani lilituumiza kichwa ila Watanzania wenye mapenzi mema na wewe walikuombea kila Saa kila dakika. Sasa wakati mwengine unaenda kuanza Maisha upya na mapya Karibu uraian tuje kupambana wote na imani Mungu anaenda kukutendea Miujiza mikubwa katika Maisha yako.

Mwanzo tuliona Ni Muda Kama hauwendi kumbe kila kitu ukimwachia Mungu siku zinakimbia kuliko kweli Mungu Ni mwema natumai @elizabethmichaelofficialumemuona Mungu ajakuacha nikuombe Nawe usimwache MUNGU.

Nichukuwe Nafasi ya kuwashukuru wote mliokuwa nasi kwenye kipindi muhimu na kigumu najuwa mlimuombea Kwa kila mtu na imani yake basi msiache kumuombea niwashukuru hata wale ambao hawakuweza kuwa Karibu nasi Ila naiman mlituombea Muda mwingi nikushukuru sana tena sana baba mkwe Mtarajiwa @majizzo we mtu unaroho ya kipekee sana mtu akikutazama Kwa nje anaweza asipate jibu Ila moyo wako Ni wakipekee sana nimejifunza kitu kutoka kwako.
na nahisi ninamaneno mengi sana Ila la Mwisho kwako @majizzo nikukumbushe tu au nisisitize ile Pete isiwe Mwisho wa safari yenu naomba taratibu za mwisho ziendelee haraka japo najuwa kwako hilo halina tatizo ili Ndoa ipite sasa........ dogo sasa yupo Huru.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.