Jibu la Ali Kiba Baada ya Mualiko wa Kuimba Wasafi Festival ,Asema Yuko Tayari Kudhamini Wasafi Festival kupitia Mo Faya

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amemjibu Diamond Platnumz kuhusu maombi yake ya kumuomba atumbuize kwenye tamasha la Wasafi Festival.
Alikiba kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amesema kuwa kwa sasa yupo bize kusambaza bidhaa za Mo Faya katika nchi mbalimbali, hivyo hatoshiriki kwenye tamasha hilo, lakini yupo tayari kuwa mdhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya.

Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.
Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfricayangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa. 
#MofayaByAlikiba
#KingKiba
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment